ABOUT TFTC

TANZANIA FILM TRAINING CENTER (TFTC)

UTANGULIZI

Tanzania Film Training center (TFTC), Ni kituo kwaajili ya mafunzo ya Filamu. Kituo hiki kimeanzishwa mwezi june 2011 na Bwana Emmanuel Myamba (Pastor), ambaye ndiye Mkurugenzi wa TFTC. Kituo kinatambulika na mamlaka halali zinazosimamia shughuli za sanaa na mafunzo hapa nchini, kwa usajili BST/4805

DIRA
Dira ya TFTC ni kukuza uelewa wa masuala ya Filamu kwa wadau wa filamu.

MALENGO YA TFTC 
Malengo ya TFTC kuwa ni kituo kitakachotoa elimu bora ya filamu itakayomuwezesha mwanafunzi kuwa mwenye uelewa bora wa kumuwezesha kujiajiri mwenyewe kwa uhakika. Tumelenga  kuzalisha waongozaji wa filamu ( Film Directors), waigizaji wa filamu ( Film Actors/ Actress), waandishi wa miswada ( Script Writers) na wahariri wa filamu ( Film Editors) wenye uelewa kuhusu filamu.

MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA TFTC

  • Uigizaji wa filamu ( Film Actors/ Actress).
  • Uongozaji wa filamu ( Film Directors).
  • Uhariri wa Filamu (Film Editors).
  • Uandishi wa miswada (Script writing).
  • Upigaji wa picha za video (Video cameras).
SIFA YA MWOMBAJI
TFTC inatoa fursa kwa yeyote anayetaka kujifunza shughuli za filamu bila kujali kigezo cha elimu, wala umri.

MUDA WA MAFUNZO
Muda wetu ni mzuri ili kutoa fursa hata kwa wale wanaofanya kazi, na kozi inachukua muda wa miezi sita (6), miezi mitatu (3) darasani na miezi mitatu (3) iliyobaki mwanafunzi anakuwa katika elimu kwa njia ya vitendo (Field).

TFTC tuko makini sana kuangalia fursa kwaajili ya wanafunzi wetu kuhakikisha hawapitwi na hizo fursa zinazotolewa na makampuni ya utengenezaji filamu ili kuzidi kuwatambulisha na wao kuonyesha uwezo wao kwa jamii.

MAFANIKIO

Mpaka sasa wanafunzi wetu wameshajifunza vyakutosha na kutumia elimu yao katika fulsa mbalimbali zilizopatikana kwao ikiwa ni pamoja na kushiriki katika filamu zifuatazo:-
  1. GOD'S KINGDOM
  2. PASUKO LA MOYO
  3. MAPITO YANGU
  4. ZERO BRAIN
  5. MY MAN
  6. ANGUKO
  7. CRAZY IN HOSPITAL
  8. SIRI YA MTUNGI (Tamthiliya)
  9. TUANGOMA ( Tamthiliya)
 Mafanikio makubwa zaidi ya TFTC ni kuwa na tawi lake Mbeya ambao nao wanafanya vizuri sana.

WALIMU
Tunatumia walimu waliobobea kutoka chuo kikuu.

Tunawakaribisha sana TFTC kwa maelezo zaidi tupigie 0712723600.